
Klabu ya Chelsea ipo katika hatua nzuri za kumnasa kiungo wa klabu ya Metalist Kharkiv ya nchini Ukraine Taison.Taison ni moja kati ya viungo bora katika Ligi kuu ya soka nchini Ukraine na kuna taarifa kuwa mchezaji huyo alikutana na mmiliki wa klabu hiyo ya Chelsea Roman Abramovich hivi karibuni katika kuhakikisha kuwa Chelsea inamtwaa kiungo huyo mshambuliaji.
Taison ataungana na wabrazil wengine kunako kikosi cha Chelsea ambao ni Ramirez,David Luiz,Lucas Piazon na Oscar endapo atasajiliwa.Anacheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji akiwa na uwezo wa kufunga,kutoa pasi na kuchezesha timu.
0 comments:
Post a Comment