
Kocha msaidizi wa Afrika Kusini Thomas Madigage amefariki dunia mara baada ya kupata ajali ya gari leo asubuhi.Taarifa ya chama cha soka nchini Afrika Kusini(SAFA) inasema kuwa ajali hiyo ya gari ilitokea katika kitongoji cha Burgesfort katika mji wa Limpopo.
"Tumeshtushwa na taarifa za kifo cha Thomas na tupo njiani kuelekea katika familia yake kujua nini kilitokea"anasema Rais wa chama cha soka nchini Afrika Kusini(SAFA) Kirsten Nematendani.Madigage anayeaminika kupata ajali hiyo wakati alipokwenda kumuona mama yake ambaye anaumwa katika maeneo ya Polokwane katika kitongoji cha Burgesfort.
0 comments:
Post a Comment