![]() |
Chamakh akiwa katika uzi mpya wa West Ham United |
Klabu ya West Ham United imeendelea kujiimarisha katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili mara baada ya kumchukua mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Morocco Marouane Chamakh.Chamakh amesaini mkataba wa miezi 6(sita) kwa mkopo katika klabu hiyo huku kukiwa na kutoridhika kwa dili hilo baina ya pande mbili za vilabu vya Arsenal na West Ham United.Katika kuonesha kuwa uhamisho huo wa Chamakh umekuwa katika utata,mtoto wa mmiliki wa klabu ya West Ham Jack Sullivan ambaye baba yake David Sullivan ndiye mmiliki ameandika katika mtandao mmoja wa kijamii kuwa "samahani sana kwa hizi taarifa kuwa Chamakh amesaini mkataba wa miezi 6(sita) tu siyo chaguo langu".
0 comments:
Post a Comment