
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu hapa
nchini, Yusuf Manji, ameingia kwenye mbio za uongozi za Shirikisho la Soka
nchini (TFF), baada ya kuchukuliwa fomu na mmiliki wa klabu ya African Lyon,
Rahim Zamunda leo katika ofisi za TFF.
Zamunda alimchukulia fomu za kuwania nafasi ya
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa nia ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza
mwenyekiti huyo wa Yanga.
Uchaguzi huo utafanyika Februari 24 huku ukizidi
kuleta msisimko wa aina yake kutokana na majina ya wanamichezo wanaojitokeza
katika patashika hiyo.
Mbali na Manji, wengineo waliochukua fomu leo ni
pamoja na Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani na Omari Mussa Nkwarulo, ambao
wamechukua fomu za kugombea urais wa TFF.
Uchaguzi wa TFF unasubiriwa kwa hamu na mashabiki
wa soka hapa nchini, ikiwa ni hatua ya kupatikana viongozi wapya, hasa baada ya
kipindi cha rais anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga kumalizika na kutangaza
kutogombea tena nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment