Jason Nono Mayele yaweza kuwa jina geni kidogo kwa watu
wengi hasa wapenzi wa soka na wale wasio wa soka.Huyu ni mchezaji wa zamani wa
vilabu vya La Berrichonne de
Châteauroux au Châteauroux) za nchini Ufaransa pia amewahi
kuvichezea vilabu vya Cagliari pamoja na
Chievo Verona za nchini Italia.Ameshawahi
pia kuichezea timu ya taifa ya Congo DRC katika miaka ya 2000 mpaka
2002.
Jason Nono Mayele alizaliwa mnamo tarehe ya 4 Januari 1976
pale Kinshasa nchini DRC Congo.Akicheza katika nafasi ya
winga/mshambuliaji,Jason alianza maisha ya soka katika klabu ya Brunoy FC ya
nchini Ufaransa kabla ya kuhamia klabu ya Chateauroux na kisha kwenda klabu ya
Cagliari kabla ya kumalizia soka lake kunako klabu ya Chievo Veron ambapo ndipo
mauti yalipomkuta.
KIFO CHAKE.
Kifo cha Jason Nono Mayele kilitokana na ajali ya gari
iliyotokea mnamo tarehe 2 Machi 2002. Jason alikuwa akitoka nyumbani kuliwahi
basi la wachezaji wa Chievo Verona kwani
timu hiyo ya Chievo ilikuwa ikijiandaa
na mechi dhidi ya klabu ya Parma katika mchezo wa Serie A pale Estadio Ernio
Tardin kunako mji wa Parma.Gari ya Jason iligongana na gari nyigine ndogo
iliyokuwa na abiria wawili mmoja akiwa mwanamke ambaye alifariki papo
hapo.Jason naye alifariki wakati akipelekwa hospitali ya Verona kwa helikopta iliyokuja haraka kumchukua mara
baada ya ajali hiyo lakini kutokana na majeraha makubwa aliyopata katika ajali
hiyo Jason aliaga dunia kabla ya kufika hospitali.
Katika kuonesha kukuguswa na msiba huo,aliyekuwa waziri wa
michezo wa wakati huo wa Congo DRC Timothee Moleka alisikika akisema kuwa “ni
ngumu kulipokea jambo hili kwani dunia ilianza kumjua Jason na hakika alikuwa
ni nyota mpya wa soka kwa Congo DRC”.Naye
mmoja kati ya waandishi wa habari za michezo nchini Congo Crispian
Selemani hakuwa nyuma katika kulizungumzia tukio hilo kwa kusema kuwa “ni tukio
la ghafla na la kusikitisha hakika ‘Simba’(jina la utani la timu ya taifa ya
Congo DRC)ilikuwa ikimtegemea mno”.
Jason Nono Mayele alionesha uwezo mkubwa sana katika fainali
za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Mali kwani aliweza kushirikiana vyema
na wachezaji kama Shabani Nonda aliyekuwa akichezea Monaco ya nchini Ufaransa
na Tresor Lua Lua aliyekuwa Newcastle United ya nchini England.Na tukio kubwa
katika fainali hizo ni timu yake ya taifa ya Congo DRC kuwatoa Tembo wa Afrika
Magharibi timu ya Ivory Coast katika hatua ya raundi ya pili na kuingia robo
fainali.
Katika kuonesha kuguswa na kifo chake,klabu ya Chievo Verona
ya nchini Italia imesitisha kuitumia jezi Namba
30 iliyokuwa ikivaliwa na nyota huyo kwa heshima yake.
KUMBUKUMBU
NA SPORTS GALLA
0 comments:
Post a Comment