![]() |
Serena William |
WACHEZAJI nyota wa tenisi Victoria Azarenka na Serena
Williams wamefanikiwa kutinga mzunguko wa pili wa michuano ya wazi ya Australia
baada ya kushinda michezo yao ya ufunguzi. Williams anayeshika namba tatu
katika orodha za ubora duniani alifanikiwa kumfunga Edina Gallovits-Hall wa
Romania kwa 6-0 6-0 pamoja na kuumia kifundo cha mguu wakati akiongoza katika
seti ya kwanza. Azarenka ambaye ni kinara katika orodha za ubora naye
alifanikiwa kuanza vyema kampeni zake za kutetea taji hilo baada ya kumfunga
Monica Niculescu pia wa Romania kwa 6-1 6-4katika mchezo wa uliochezwa katika
Uwanja wa Rod Laver Arena jijini Melbourne. Kwa upande wanaume Andy Murray
a mbaye anashika namba tatu katika orodha za ubora alifanikiwa kuanza vyema
michuano hiyo kutafuta taji la pili la Grand Slam baada ya kumfunga Robin Haase
wa Uholanzi kwa 6-3 6-1 6-3. Wakati Roger Federer ambaye ni bingwa mara
nne wa michuano hiyo naye alisonga mbele baada ya kumsambaratisha mfaransa
Benoit Paire 6-2 6-4 6-1 akitumia muda wa saa moja na dakika 23.
0 comments:
Post a Comment