
Klabu ya Liverpool imeendeleza wimbi la ushindi mara baada ya kuifunga timu ya Sunderland kwa magoli 3-0.Mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Anfield ilimshuhudia mshambuliaji Luis Suarez akifunga magoli mawili peke yake huku goli lingine likifungwa na kinda Raheem Sterling.Ulikuwa ushindi muhimu kwa kocha Brendan Rodgers wa Liverpool kwani ndani ya siku nne ameshinda mechi mbili za Ligi ya England.

Katika dimba la Stanford Bridge,klabu ya Chelsea ilikubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya klabu ya QPR.Goli la ushindi la QPR lilifungwa na mchezaji Shaun Wright-Philips ambaye amekwishawahi kuichezea klabu hiyo ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment