![]() |
Abigail akiwa na Obafemi Martins |
Taarifa za ndani toka katika mitandano ya kijamii zinasema kuwa mshambuliaji wa Manchester city Mario Balotelli ataitwa mjomba hivi karibuni mara baada ya kugundulika kuwa dada yake Abigail Barwuah Balotelli ni mjamzito akiwa na mimba ya mchezaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan na Newcastle ambaye anaichezea klabu ya Levante Obafemi Martins.
Kwa mujibu wa gazeti la 'Diva e Dona' la nchini Italia lilimnukuu Abigail akisema kuwa"ni furaha kupata taarifa za mtoto kwa wakati huu na sikukuu ya Chrismass itakuwa nzuri sana(mwaka jana).Mwezi uliopita aliyekuwa rafiki wa kike wa Balotelli Raffaella Rico alijifungua mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Pia amabye hata hivyo mchezaji huyo alimkataa mpaka mtoto huyo atakapochukuliwa vinasaba(DNA) katika kuthibitisha uhalali wa mtoto huyo kwa Balotelli
0 comments:
Post a Comment