
Beki wa kati wa klabu ya Atalanta Bergamo ya nchini Italia Federico Peluso anafanyiwa vipimo leo ili kukamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Juventus kwa msimu huu wa 2012-13.Peluso anayetajwa kuwa mmoja kati ya mabeki bora wa kati katika Ligi Kuu ya soka nchini Italia atajiunga na mabingwa hao wa Italia mara tu atakapokamilisha vipimo vyake vya afya.
Federico Peluso yawezakana likawa jina geni katika masikio ya wengi lakini ndiye anayeonekana anaweza kuwa mbadala wa beki aliyeumia Giorgio Chiellin ambaye atakosekana kwa muda wa miezi mitatu.Ni mchezaji ambaye amekulia katika kituo cha kulelea vijana cha Lazio lakini akapata kuvichezea vilabu vya Pro Vercelli,Ternana,AlbinoLeffe na Atalanta Bergamo klabu ambayo amichezea zaidi ya mechi 100.Uhamisho wa Peluso utakuwa wa mkopo kwenda klabu ya Juventus.
0 comments:
Post a Comment