
COASTAL Union ya Tanga imelazimishwa sare ya
kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro, katika mchezo wa Kundi B Kombe
la Mapinduzi, jioni hii kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona
lango la mwenzake na Coastal Union ndio walitakiwa kujilaumu kwa kushindwa
kutumia mwanya wa Mtibwa Sugar kucheza pungufu kutokana na beki wake, Salum
Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43.
Timu zilishambuliana kwa zamu katika kipindi hicho,
upande wa Coastal ukiongozwa na Danny Lyanga na Mtibwa Hussein Javu.
Baada ya Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu,
kocha Mecky Mexime alimuinua beki Rajab
Mohamed kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji,
Hassan Seif.
Kipindi cha pili, Mtibwa walirudi kwa kasi na
kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 58, mfungaji Ally Mohamed ‘Gaucho’
aliyepiga shuti la umbali wa mita 19 na kumtungua Juma Mpongo.
Coastal Union ilisawazisha bao hilo dakika ya 81,
mfungaji Jerry Santo aliyefumua shuti la chini la umbali wa mita 24 na
kumtungua kipa Hussein Sharrif.
Katika mchezo huo, kikosi cha Mtibwa Sugar
kilikuwa; Hussein Sharrif, Hamisi Issa, Yussuf Nguya, Salvatory Ntebe, Salum
Swedi, Babu Ally Seif, Ally Mohamed ‘Gaucho’, Rashid Gumbo, Hussein Javu,
Hassan Seif/Rajab Mohamed dk43 na Vincent Barnabas.
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman
Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim
‘Selembe’, Jerry Santo, Mohamed Miraj, Mohamed Soud Othman na Danny
Lyanga.
0 comments:
Post a Comment