CHAMA
cha Mpira wa Miguu Ilala (IDFA), kimeandaa kozi ya waamuzi itakayofanyika
Januari 25, katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
Kozi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kutafuta waamuzi
wapya watakaoandaliwa vyema na kutumiwa siku za usoni, hasa kwa wale vijana
wadogo, huku ikipangwa kufanyika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa muda
wa mwezi mmoja.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu
wa Chama hicho, Kanuti Daudi, alisema kwamba hadi sasa wameshajiandikisha
vijana 20 wenye lengo la kushiriki kozi hiyo ya waamuzi.
Alisema bado nafasi zipo kwa wale wanaohitaji kozi
hiyo, huku wakiamini kuwa italeta tija na kuinua michezo kwa kuwa na waamuzi
bora.
"Tumeamua kuandaa kozi ya waamuzi kwa ajili ya
kutafuta watu wa kuendeleza zaidi michezo hasa mpira wa miguu, kwa kuhakikisha
mambo yanakwenda sawa.
"Naamini mambo yatakuwa mazuri hasa kwa wale
vijana watakaojitokeza zaidi kwakuwa bado nafasi zipo na tunaamini watashiriki
kwa wingi," alisema.
DRFA ni chama kinachopigania maendeleo ya mpira wa
miguu Ilala, huku timu kongwe na zenye mashabiki wengi, ikiwamo Simba na Yanga
zinazotokea katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment