Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, December 27, 2012

SIMBA KUWAVAA TUSKER KOMBE LA MAPINDUZI

http://1.bp.blogspot.com/-Bx84k0ZShWg/T6QIRH8bh9I/AAAAAAAAAs0/XpYavJefeEY/s1600/1.JPG
Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi imetoka rasmi huku  klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imepangwa kundi moja na timu ya Tusker FC toka nchini Kenya.Kombe la Mapinduzi lilianzishwa rasmi na Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kwa kumbukumbu ya Mapinduzi yaliyofanyika visiwani humo tarehe 12 mwezi Januari mwaka 1963 na hivyo huandaa michuano hiyo kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya tukio hilo.

Katika kuleta ladha ya michuano hiyo ,Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA)walipeleka mualiko kwa timu za Al Ahly(Misri) na APR (Rwanda) lakini kutokana na sababu kadha wa kadha,timu hizo hazitashiriki.Pia mabingwa wa Kombe la Kagame klabu ya Yanga nayo haitashiriki kwani itakuwa safarini nchini Uturuki katika kambi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

Azam ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza tarehe 2 Januari mpaka tarehe 12 ya mwezi huo.Mshindi wa michuano hiyo atapata dola za kimarekani $6400(Tsh 10mil) wakati mshindi wa pili atapata dola $3200 (Tsh 5mil).

Makundi ya michuano hiyo ni:

Group A: Simba SC, Tusker FC, Bandari (Unguja) and Jamhuri (Pemba).
Group B: Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union, and Miembeni (Unguja)

0 comments:

Post a Comment