
Mchezaji wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Juventus Kwadwo Asamoah amesema kuwa alipata shida mno kucheza katika nafasi ya beki wa kushoto na kitumika pia kama winga (wingbeck) kwa mara ya kwanza akiwa na klabu ya Juventus kwani alizoea kucheza kama kiungo wakati akiwa na klabu ya Udinese.Akizungumza na kituo cha runinga kinachoitwa Tv3, Kwadwo anasema kuwa 'haikuwa rahisi wakati najiunga na Juve kucheza nafasi ya beki na kiungo katika kikosi cha kwanza ingawa kwa sasa nimezoea hali hiyo'.
Asamoah ndiye mchezaji pekee wa Juve aliyecheza mechi nyingi mpaka sasa kwani amekwishacheza mechi 25 katika mashindano yote ambayo klabu ya Juventus inashiriki zikiwepo mechi 18 za Serie A msimu huu.Asamoah anamalizia kwa kueleza siri ya mafanikio yake katika kikosi hicho nayo ni kujituma na kufanya mazoezi kwa nguvu.
0 comments:
Post a Comment