
Mchezaji Danny Shittu anayecheza nafasi ya ulinzi kunako klabu ya Millwall ya Ligi daraja la kwanza nchini England ameandika barua rasmi kwa chama cha soka nchini Nigeria (NFF) kuwa hatokuwepo katika fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika ya Kusini.Shittu aliyejumiushwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 32 cha Nigeria cha kocha Stephen Keshi alituma ujumbe wa barua pepe (Email) kwa chama hicho cha soka nchini Nigeria ya kujiondoa katika kikosi hicho maarufu kama 'Super Eagles'.
Akizungumzia suala la mchezaji huyo,mjumbe wa kamati kuu wa chama cha soka nchini Nigeria Barrister Chris Green anasema kuwa 'ndiyo,tumepokea barua pepe toka kwa mchezaji Danny Shittu lakini bado tunayasoma mazingira na hatutaweza kutoa tamko lolote kwa sasa mpaka tutakapojiridhisha kwa kile tutakachokiona.Wakati huohuo meneja wa klabu ya Millwall Kenny Jackett alihaidi wiki iliyopita kumshawishi mchezaji huyo abaki na timu yake ya Millwall ambayo ni nahodha msaidizi.
0 comments:
Post a Comment