
Klabu ya Tusker ya nchini Kenya imeifunga klabu ya Simba kwa magoli 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Magoli ya Tusker katika mchezo huo yalifungwa na Jesse Were aliyefunga magoli mawili(2) katika dakika za 37 na 44 na kuifanya Tusker iongoze kwa magoli 2-0 mpaka mapumziko.Frederick Onyango alifunga goli la 3 na la mwisho kwa Tusker.
0 comments:
Post a Comment