Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, December 29, 2012

KUELEKEA MATAIFA YA AFRIKA: KOCHA ETHIOPIA AACHA WACHEZAJI 5


 

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Ethiopia Sewnet Bishaw amewaacha wachezaji watano katika kikosi kilichokuwa na wachezaji 31 na sasa kikosi hicho cha 'wahabeshi' kubaki na wachezaji 26 tu.Taarifa rasmi zinasema kuwa kocha huyo atapunguza wachezaji wengine 3 mara baada ya kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu za Niger,Tunisia na Guinnea na kubaki na wachezaji 23 tu tayari kwa michauno ya mataifa ya Afrika mwakani 2013 nchini Afrika Kusini.

Wachezaji walioachwa ni mjumuisho wa wachezaji 4 wanaocheza Ligi ya ndani ya mmoja anayecheza nje ya Ethiopia.Wachezaji walioachwa ni pamoja na Fitsum Mariam (St.George),Fitsum Feteri (Commercial Bank),Mulualem Mesfin (Arba Minch City),Medhane Tadesse (Defence Force) na David Beshah (TSC Euskirchen,German).Timu hiyo imefuzu fainali hizo mwaka huu ikiwa ni miaka 31 tangu wafanye hivyo mwaka 1981.Ethiopia wamepangwa kundi C pamoja na mabibgwa watetezi Zambia,Nigeria na Burkina Faso.

0 comments:

Post a Comment