Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, December 29, 2012

MAN CITY,MAN UNITED NA ARSENAL ZASHINDA EPL

 Game over: Robin van Persie celebrates scoring his team's second goal
Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea tena leo ambapo mechi takribani nane zilipigwa kunako viwanja tofauti tofauti.Kule Old Trafford kunako jijni la Manchester,klabu ya Man United iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 mbele ya vijana wa Steve Clarke West Bromwich Albion.Magoli ya Man United yalifungwa na mchezaji wa WBA Gareth McAuley aliyejifunga na baadaye mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Robin Van Persie akifunga goli la pili likiwa ni goli la 17 kwake tangu msimu huu uanze na mwisho wa siku ni United kupata ushindi wa magoli 2-0. dhidi ya WBA.
Star of the show: Edin Dzeko scored within two minutes for Manchester City
Kule Carrow Road klabu ya Manchester City iliivurumisha klabu ya Norwich City kwa magoli 4-3 pambano lililokuwa kali na la kusismua sana.Norwich ni moja kati ya vilabu vigumu sana kufungika msimu huu na hakika wamekuwa wakitoa upinzani mkubwa sana kwa vilabu vingine vya Ligi kuu nchini England pindi vinapodhuru katika uwanja wa Carrow Road.Alikuwa ni mshambuliaji Edin Dzeko aliyefunga mara mbili huku magoli mengine ya City yakifungwa na Kun Aguero na goli la kujifunga la golikipa wa Norwich City Bunn.
Spicy: Samir Nasri was red-carded for putting his head against Sebastien Bassong's
Magoli kwa upande wa Norwich City yalifungwa na wachezaji Pilkington na Martin aliyefunga magoli 2.Katika pambano hilo mchezaji Samir Nasri alipewa kadi nyekundu kwa kosa la kumwekea kichwa mchezaji Sebastian Bassong na hivyo mwamuzi Mike Jones kumuonesha Nasri kadi nyekundu.
Middle man: Theo Walcott scored a brilliant hat-trick as Arsenal thumped seven past a hapless Newcastle
Pale Emirates alikuwa ni mchezaji Theo Walcott aliyekuwa shujaa wa Arsenal mara baada ya kufunga peke yake magoli 3 katika ushindi walioupata klabu ya Arsenal dhidi ya klabu ya Newcastle United wa magoli 7-3.Magoli ya Arsenal yalifungwa na Walcott(3),Giroud(2),Oxlaide Chamberlain na Podolski huku magoli ya Newcastle yakifungwa na Demba Ba (20) na Marveaux akifunga goli 1.

Matokeo mengine:

  • Sundeland 1-2 Tottenham
  • Stoke City 3-3 Southampton
  • Aston Villa 0-3 Wigan

0 comments:

Post a Comment