Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, December 27, 2012

FIGO:RONALDO ANASTAHILI BALLON D'OR

 Figo y Cristiano
Mchezaji wa zamani nguli kunako vilabu mbalimbali vya FC Barcelona,Real Madrid,Inter Milan na timu ya taifa ya Ureno Luis Figo anasema kuwa mchezaji Cristiano Ronaldo anastahili tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ijulikanayo kama FIFA Ballon d'or.Figo anasema kuwa 'hakuna kitu cha kumzuia Ronaldo hasiwe mwanasoka bora wa dunia kwani amefanya makubwa sana kwa klabu yake ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno kwa mwaka huu (2012).

Figo hakusita pia kuonesha ushindani uliopo katika tuzo hizo kwa kuangalia uwepo wa wachezaji wengine ambao nao wamekuwa wakifanya vizuri katika klabu yao ya Barcelona nao si wengine bali ni Lionel Messi na Andres Iniesta.Messi ana rekodi nzuri sana kwani pamoja na hali iliyopo ya kujitokeza wachezaji wengi wa zamani kuwa ndiyo wameweka rekodi ya ufungaji wa magoli mengi kwa mwaka lakini ukweli unabaki kuwa ndiye aliyefunga magoli mengi kwa mwaka huu 2012 kwa kufikisha idadi ya magoli 91 akivunja rekodi  iliyokuwa ikishikiliwa na mchezaji Gerd Muller ambaye pia anajulikana kama 'The Bomber of the Nation' ambaye alifunga magoli 85 kwa mwaka mmoja.

Figo ambaye alipata tuzo hiyo mwaka 2000 anasema kuwa wakati wake alifurahi kupata tuzo hiyo kwani ushindani ulikuwa mkubwa sana tofauti na sasa ambapo ushindani upo kwa wachezaji wanne mpaka watano ambao ndiyo wanaovuma duniani.

0 comments:

Post a Comment