
Magoli ya mawili yaliyowekwa kimiani na kiungo nyota kunako klabu ya Chelsea Frank Lampard yaliipa ushindi timu hiyo ya Chelsea na hivyo kuifanya isogee mpaka katika nafasi ya tatu ikiwa na point 38 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.Everton walianza mechi kwa kasi kwani kunako dk ya 1 kwanza tu ya mchezo kiungo Steven Pienaar alianza kufunga kwa upande wa Everton lakini baadaye kiungo wa Chelsea Frank Lampard alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 42 na baadaye kunako dk ya 72 kiungo huyo alifunga tena na hivyo kuihakikishia ushindi klabu hiyo ya darajani.

Kule Loftus Road klabu ya Liverpool jana iliweza kuzinduka na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya klabu ya QPR.Katika pambano hilo mshambuliaji Luis Suarez aliweza kufunga magoli mawili huku beki wa kati Daniel Agger akifunga goli lingine.
0 comments:
Post a Comment