
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya filimbi ya kuashiria kuanza kwa mataifa ya Afrika haijapulizwa,nchi mbalimbali zinazoshiriki michuano hiyo zipo katika hatua ya mwisho ya maandalizi kwa kucheza mechi za kirafiki kujiandaa na fainali hizo.Timu ya Tunisia jana iliweza kuifunga timu ya Iraq kwa magoli 2-1.Magoli ya ya Tunisia yalifungwa na Issam Jemaa na Fakhreddine Ben Youssef huku goli la Iraq likifungwa na Younes Mahmoud pambano likipigwa pale international kunako mji wa Sharjah.Tunisia imeweka kambi yake Dubai na inatarajiwa kufungua na timu ya taifa ya Algeria mnamo Januari 22 mwakani (2013).
0 comments:
Post a Comment