Kocha mpya wa Simba, Mfaransa,
Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa
saba za mchana kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba. Uongozi wa Simba, kwa kupitia
Katibu Mkuu wao, Evodius Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo
waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Kocha huyo anawasili huku
akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo Julio, kocha ambaye
amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa kitendo chake cha
kukubali kuinoa timu hiyo.
Mengi juu ya ujio wa kocha huyo
raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo ya mwisho na kuingia
makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa cha kurudisha imani
kwa wapenzi na wanachama wao.
Simba ilimaliza mzunguko wa
kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu, nyuma ya timu ya Yanga
na Azam FC.
0 comments:
Post a Comment