Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, November 6, 2012

XABI ALONSO NDIYYE KIUNGO WANGU BORA-GERRARD

Nahodha wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard amesema kuwa kiungo wa sasa Real Madrid Xabi Alonso ndiye mchezaji wake bora katika nafasi ya kiungo ambaye alibahatika kucheza naye timu moja ya Liverpool.Gerrard aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwa ushirkiano na kampuni ya vifaa vya michezo vya Adidas.

Katika tukio lingine,nahodha huyo wa timu ya Liverpool pamoja na timu ya taifa ya England alimtaja mshambuliaji Luis Suarez kama mmoja kati ya washambuliaji wake bora aliopata kucheza nao katika timu ya Liverpool.Gerrad anasema kuwa Suarez ni bora zaidi ya wachezaji nyota ambao yeye Gerrard alipata kucheza nao kama Robbie Fowler,Michael Owen pamoja na Fernando Torres.

0 comments:

Post a Comment