Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, November 5, 2012

SANTOS AOMBA MSAMAHA SAKAT LA KUBADILISHANA JEZI NA VAN PERSIE

Mchezaji Andre Santos amewaomba msamaha mashabiki wa klabu yake ya  Arsenal kutokana na kitendo chake cha kubadilishana jezi na mchezaji Robin Van Persie katika mechi yao(Arsenal dhidi ya Man United) jijini Manchester.Katika mechi hiyo iliyoisha kwa Man United kushinda magoli 2-1 iliwafanya mashabiki wa Arsenal kumzomea mchezaji huyo amabye anacheza nafasi ya beki wa kushoto  kutokana na kitendo hicho.

Katika taarifa yake kwa mashabiki mchezaji huyo ameomba msamaha kwa mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa wazo la kubadilishana jezi lilikuwa ni la Van Persie mwenyewe hivyo yeye kujikuta akiipokea jezi ya nyota huyo na kisha kumpa yake kama ishara ya 'Fair Play'.Andre Santos amejumuishwa katika kikosi cha cha Arsenal kilichosafiri kwenda Ujerumani kupambana na Schalke 04 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya leo usiku.

0 comments:

Post a Comment