
Magoli ya Mathew Valbuena na Batefimbi Gomez yalitosha kuwanyamazisha wataliano katika mechi ya kirafiki ya kimataifa katika pambano kali na la kusisimua kunako uwanja wa Estadio Ennio Tardin katika jiji la Parma.Lilikuwa ni pambano la kukata na shoka ambapo timu zote mbili ziliwachezesha wachezaji chipukizi na hivyo kuleta msisimko katika pambano hilo.Wachezaji kama Stephen El Shawary,Balloteli.Marco Vellati,Giovinco walianza kwa upande wa Italia huku Olivier Giroud,Batefimbi Gomez,Laurent Koscienly na Mathew Debuchy walicheza kwa upande wa Ufaransa.Katika pambano hilo Ufaransa walishinda magoli 2-1 kwa magoli ya Mathew Valbuena na Batefimbi Gomez huku mchezaji Stephen El Sharawaay akifunga kwa upande wa Italia.
0 comments:
Post a Comment