Hakika alitabiriwa kuwa na maisha
mazuri na marefu katika mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA
kutokana na kushika nafasi ya pili katika ile iliyoitwa NBA College Draft
ambayo hufanyika kila mwaka hasa kwa wale wanafunzi wa vyuo vikuu ambao hucheza
mpira wa kikabu au Basketball.Si mwingine bali ni Mtanzania mwenzetu Hasheem
Thabeet.
Hasheem Thabeet alichaguliwa katika katika
timu ya Memphis Grizzliers akiwa kama mshindi wa pil wa NBA draft ya mwaka 2009
na hapo ndipo maisha ya kijana huyu Mtanzania yalipoanza katika ulimwengu wa
mpira wa kikapu.Tangu achaguliwe katika timu ya Memphis Grizzlies,Hasheem hakuwahi
kufanya vizuri katika timu hiyo na hivyo kuzusha maswali mengi kuwa kama kweli
ni huyu Haseem aliyeshika nafasi ya pili katika draft ya NBA au la.
Msimu huu wa kikapu wa mwaka
2012-13,Hasheem Thabeet amechukuliwa na timu ya Oklahoma City Thunder akitokea
Houston Rocket timu ambayo hakufanya pia vizuri wakati akitokea timu ya Memphis
Grizzlies.Wataalamu wa mambo wanasema kuwa kwa Hasheem Thabeet kwenda
OklahomaCity Thunder kutamfanya kijana huyu wa kitanzania kung’ara katika Ligi
Kuu ya kikapu nchini Marekani.
Kung’aa kwa Hasheem kutatokana na mambo
mengi lakini kati ya hayo ni timu ya Oklahoma kuwa na uongozi mzuri uliojipanga
katika kufanya mapinduzi makubwa katika timu hiyo na Ligi kuu ya NBA kwa ujumla
chini ya kocha Sam Presti.Sam Presti ana kipaji cha kuendeleza vijana wenye
vipaji kwa kuwachanganya na nyota wengine katika timu anayofundisha hivyo
haitakuwa tabu kwa mchezaji mwenye futi 7’3 kama Hasheem kufanya vyema katika
NBA.
Ni kweli mpaka sasa Hasheem hajawa
na misimu mizuri katika NBA kwani hata rekodi zake zinaonesha hivyo.Kwa mfano
tangu Hasheem aingie NBA ameanza michezo 16 tu huku muda mwingi akiutumia
katika Ligi ya vijana inayotambulika kama D-League kuliko Ligi ya wakubwa yani Ligi
ya Shirikisho(NBA).
Katika Ligi ya wakubwa yani NBA kwa
mwaka 2009 mpaka 2012 Hasheem alikuwa na wastani pointi 2.2,rebounds 2.7,pasi
za magoli 0.1,akiiba mipira kwa wastani wa 0.2 na akizuia mipira kwa wastani wa
0.9 kwa kila mchezo akiwa na ile PER(Players Efficenty Rating) ya 10.7.Hizi
siyo takwimu mbaya kwa mchezaji wa kariba ya Hasheem na ndiyo sababu ya kocha
Presti kuamua kumchukua Hasheem katika kikosi cha Oklahoma City Thunder.
Hasheem hatopewa majukumu makubwa
sana katika timu ya Oklahoma bali kikubwa ambacho mwalimu Presti anakitegema toka kwa Hasheem ni kucheza kama mlinzi katika
kuzuia mpira inayokwenda katika goli au kikapu(shots) au rebounds kwa maana ya
ile mipira inayozagaa katika lango la Oklahoma. Sidhani kama pia atakuwa
akianza katika kikosi cha kwanza kikiwa na nyota kama Kelvin Martin,Kelvin Durant
na Russel Westbrook.
Akiwa na timu ya Connecticut
hakufanya mabo mengi sana zidi ya hayo niliyoyataja.Hakuitaji kuwa mfungaji
alikuwa bora katika eneo alilocheza la ulinzi.Ni vizuri kukumbuka kuwa kikubwa
kinachomfanya mchezaji kuwa bora katika NBA ni kujituma na kucheza kwa bidii na
hilo halina shaka kuwa Hasheem anaweza kulifanya akiwa na Oklahoma City Thunder
.
0 comments:
Post a Comment