Ilikuwa ni Tarehe 25 November 1992 siku ya Jumatano mchezaji Daniel Amokachi
alifunga goli katika dakika ya 17 katika pambano kali na la kusisimua kati ya Club Brugge ya
(Ubelgiji) dhidi ya CSKA Moscow ya nchini (Urusi) .Pambano hilo Ilikuwa ni
kuashiria kuanza kwa mashindano mapya ya ulaya yaliyojulikana na yanayojulikana
kama Klabu Bingwa Ulaya.Hakika bara la Ulaya lilikuwa katika nuru mpya katika
soka kwani hapo kabla watu walishuhudia michuano hiyo ikijulikana kama Kombe la
washindi barani Ulaya na tangu wakati huo wa 1992 mpaka sasa ni Klabu Bingwa
Ulaya.Tarehe kama hiyo na mwezi kama huo mwaka huu (2012) itakuwa ni miaka 20 ya kuanzishwa kwa Klabu Bingwa Ulaya
Ni michuano ambayo ilikuwa na maswali mengi kwani baadhi ya
vilabu vikubwa wakati huo vilikosekana kutokana na kutolewa katika hatua za
awali kwenye miezi ya Septemba na Oktoba.Vilabu hivyo ni pamoja na Leeds
United(England),FC Barcelona(Spain) bila kusahau VFB Stuttgartya nchini
(Ujerumani) na hivyo watu kuamini kuwa michuano hiyo haiwezi kufana lakini
kiukweli ilifana na inaendelea kufana sana.
Mwaka huu fainali ya UEFA au Klabu Bingwa Ulaya itafanyika
katika dimba la Wembley ikiwa ni maadhimisho ya miaka takribani 20 tangu
ijulikane kama Klabu Bingwa Ulaya.Mambo mengi au kuna mabadiliko mengi hapa
katikati tumeyashuhudia lakini kubwa katika hayo ni matangazo ya televisheni
kwa michauno hiyo kwani kwa kiasi kikubwa yamezidi kuleta msisimko na pia
kuzidi kulipa utajiri shirikisho la soka Barani Ulaya pamoja na vilabu shiriki
katika michuano hiyo.
Hivyo kuelekea
michezo ya kesho(Jumanne na Jumatano)ya Klabu Bingwa Ulaya,zimebaki siku saba
tu za kusheherekea michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992.Ni miaka 20
ya michuano hiyo na hakika UEFA kama Shirikisho la soka Barani Ulaya
wanastahili pongezi kwa hilo.
Gianni Ifantino
Katibu Mkuu UEFA
0 comments:
Post a Comment