Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, November 8, 2012

MTOTO WA MESSI AWA LULU

Zikiwa ni siku sita tu tangu kuzaliwa kwake,mtoto wa mchezaji nyota wa dunia Lionel Messi Thiago Messi ameanza kuwa lulu kwa vilabu na makampuni ya masoko duniani katika kile kinachoitwa kuwa atakuwa nyota kama baba yake hapo badaye.Tayari klabu ya Newell's Old Boys ya nchini Argentina aliyokulia Messi imempa mtoto wake huyo Thiago kadi maalum ya uanachama wa klabu hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kumfanya mtoto huyo aje kuwa nyota wa timu hiyo na timu ya taifa ya Argentina.

Mtoto Thiago alizaliwa Novemba 2 mwaka huu na tayari klabu ya Newell's imeshachapisha jezi namba 10 na tayari imetoa kadi namba 288152-1 katika klabu hiyo ya Rosario alipokulia mchezaji Messi na wachezaji wengine nyota kama Gabriel  Batistuta na Gabriel Heinze.

0 comments:

Post a Comment