Klabu ya Bayern imepata ushindi wa magoli 6-1 dhidi ya klabu ya Lille Metropole ya nchini Ufaransa.Alikuwa mchezaji Claudio Pizzaro ambaye alipachika magoli 3 maarufu kama 'hat-trik' huku magoli mengine yakifungwa na wachezaji Toni Kroos,Bastian Schweinsteiger na Arjen Robben.Goli pekee la Lille lilifungwa na Solomon Kalou.
Klabu ya Juventus nayo ilijiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya mtoano mara baada ya kuifunga timu ya Nordsjaelland kwa magoli 4-0 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.Magoli ya Juventus yalifungwa na Claudio Marchisio,Arturo Vidal,Sebastian Giovinco na Fabio Quagrallela.
0 comments:
Post a Comment