Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Sunday, November 4, 2012

INTER YASITISHA REKODI YA MECHI 50 BILA YA KUFUNGWA YA YUVENTUS

Punisher: Inter hitman Diego Milito struck twice
Hatimaye klabu ya Inter Milan jana ilisitisha rekodi ya klabu ya Juvenus ya kucheza mechi 50 bila ya kufungwa katika pambano lililochezwa pale Juventus Arena.Alikuwa ni Alberto Diego Milito aliyepachika magoli mawili huku Palicios akifunga lingine katika ushindi wa magoli 3-1 waliopata Inter dhidi ya Juventus.
Great start: Arturo Vidal struck in the first minute
Juventus walianza kwa kasi sana katika mechi ya jana na iliwachukua sekunde ya 22 kupata goli kupitia kwa Artulo Vidal moja kati ya viungo bora sana kwa sasa katika Serie A.Mpaka mapumziko Juve walikuwa wakiongoza kwa goli 1 lakini mambo yakabadilika kipindi cha pili mara baada ya Inter kuongeza presha kwa klabu ya Juve kupitia kwa wachezaji wake Cambiasso,Milito na Palicios bila kumsahau Cassano.
Stretch: Gianluci Buffon is beaten
Inter walipata magoli hayo kwa njia ya penati iliyofungwa na Milito kabla ya Milito tena kumalizia mpira uliotemwa na kipa Buffon kutokana na shuti kali la Fred Guarin.Palacios aliihakikishia Inter ushindi baada ya kufunga goli la tatu.Mpaka mwisho wa mchezo Inter alishinda magoli3-1.

0 comments:

Post a Comment