Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, November 7, 2012

BARCA YAKUBALI KIPIGO MBELE YA CELTIC

Ilikuwa ni miaka 125 tangu kuanzishwa kwake klabu ya Glasgow Celtic ambapo jana iliweza kuushangaza ulimwengu kwa kuifunga timu ya Barcelona kwa magoli 2-1.Hakuna aliyeamini kilichotokea mara baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Kuipers.Celtic wanarudia yale waliyoyafanya mwaka 2004 katika michuano ya Ulaya kunako uwanja huohuo wa Celtic Park mara baada yakuwafunga mabingwa hao wa zamani wa Ulaya goli 1-0  katika michuano ya UEFA Cup.Katika pambano hili magoli ya Celtic yalifungwa na Mkenya Victor Wanyama katika dakika ya 21 na kiungo Antony Watt dakika ya 83 kabla ya Lionel Messi kufunga kwa Barcelona katika dakika za majeruhi kunako dakika ya 91.

Zifuatazao ni mechi ambazo Celtic wallibuka na ushindi wa kihistoria.

    • Klabu Bingwa Ulaya , Novemba 21 2006:  Celtic 1-0 Man United goli la Shunsuke Nakamura kwa njia ya adhabu ndogo.
    • Klabu Bingwa Ulaya Oktoba 3 2007: Celtic 2-1 AC Milan huku Kaka akifunga kwa upande wa AC Milan mara baada ya Celtic kufunga kupita kwa wachezaji wake Stephen McManus na Scott McDonard.
    • UEFA cup March 11 2004,Celtic 1-0 Barcelona,goli la Alan Thompson huku mechi hiyo ikishuhudia kadi tatu za nyekundu kwa wachezaji Rab Douglas wa Celtic na Javier Saviola na Thiago Motta wa Barcelona.
    • UEFA cup March 23 2003,Liverpool 0-2 Celtic,huku Celtic wakipata ushindi wa jumla wa magoli 3-1.Magoli ya Celtic yalifungwa na Alan Thompson na John Hartson.
    • European cup, May 25 1967-Celtic 2-1Inter Milan,mechi hii iliifanya klabu ya Celtic kuwa klabu ya kwanza toka nchini Uingereza kushinda kombe la Ligi ya Ulaya kwa kuwafunga Inter Milan magoli 2-1 kwa magoli ya Tommy Gemmell na Stevie Chalmers.
    • European cup,Apr 15 1970 - Celtic 2 Leeds 1 katika mechi iliyoudhuriwa na watazamaji 138,000 pale Hampdern Park.

0 comments:

Post a Comment