
Timu ya Young Africans imepata point 3 muhimu na kushika nafasi ya 2 katika msimo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuichapa timu ya JKT Oljoro bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Yanga ambayo iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka point 3 muhimu, imefanikiwa kupata point hizo ambazo moja kwa moja zinaipeleka mpaka katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
JKT Oljoro walianza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka ushindi wa mapema, lakini umakini wa walinzi wa Yanga ulikwamisha jitihada hizo
Mchezo uliewndelea na katika dakika ya 15 ya mchezo Saimon Msuva na Hamis Kiiza katikadakika ya 21, walikosa mabao ya wazi baada ya kushindwa pasi za Didier Kavumbagu na Haruna Niyonzima.
Yanga iliendelea kucheza kwa nguvu ili waweze kupata bao la kuongoza lakini Uwanja wa Sheik Amri Abeid ulikuwa kikwazao kwa wachezaji kwani hawakuweza kucheza vizuri kutongana na mashimo na mabonde yaliyopo katika sehemu ya kuchezea.
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, JKT Oljoro 0 - 0 Young Africans
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusaka bao la mapema lakini mshika kibendera namba 2 hakuwa makini hali iliyopelekea wachezaji wa Yanga kushindwa kulifikia lango la JKT Oljoro.
Dakika ya 53, Mlinzi Mbuyu Twite aliipatia Young Africans bao la kwanza baada ya kumalizia mipra wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima, na mfungaji kuukwamisha wavuni na ubao kusomeka JKT Oljoro 0 - 1 Young Africans.
JKT Oljoro walifanya mabadiliko ya haraka haraka ili waweze kupata bao la kusawazsiha lakini mpaka umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa kikwazo.
Yanga iliendelea kukosa mabao ya wazi kupitia kwa washambuliaji wake Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu na Saimon Msuva lakini umaliziaji haukuwa mzuri kutoka na uwanja kutokua mzuri, kwani mipango yao mingi ilikwamishwa na uwanja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, JKT Oljoro 0 - 1 Young Africans - 2
Matokeo hayo yanaipeleka Young Africans mpaka katika nafasi ya 2 ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kufikisha point 20.
Yanga itacheza na JKT Mgambo siku ya jumatanokatika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 11
Yanga : 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Shadrack Nsajigwa, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Mbuyu Twite, 6.Athumani Idd 'Chuji' 7.Saimon Msuva , 8.Frank Domayo/Nurdin Bakari, 9.Didier Kavumbagu/Jeryson Tegete, 10.Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima
0 comments:
Post a Comment