
imeichapa timu ya Ruvu Shooting mabao 3-2, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ambayo iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka point 3 muhimu, imefanikiwa kupata point hizo ambazo moja kwa moja zinaipeleka mpaka katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting walianza mchezo kwa kasi na katika dakika ya pili tu ya mchezo, uzembe wa walinzi wa Yanga uliipelekea timu ya Ruvu kujipatia bao lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Seif Abdallah.
Huku Yanga ikicheza kwa nguvu ili iweze kupata bao la kusawazisha, Seif Abdallah tena aliipatia Ruvu Shooting bao la pili kwa kumalizia krosi iliyopigwa mshambuliaji wa pembeni Raphael Kyala.
Yanga ilibadili mchezo na katika dakika ya 20 ya mchezo, mlinzi Mbuyu Twite aliipatia bao la kwanza kwa njai ya faulo ya mbali mita 30, baada ya walinzi wa Ruvu kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu.
Vijana wa Jangwani waliendelea kulishambulia kwa kasi lango la Ruvu na katika dakika ya 25 ya mchezo, golikipa wa Ruvu Benjamin Haule aliomba kupatiwa matibabu kufuatia kuumizwa na mashuti ya faulo ya Mbuyu Twite.
Jeryson Tegete aliipatia Yanga bao la pili na kusawazisha, kufuatia kumalizia kazi nzuri iliyofanya na Haruna Niyonzima.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika, Young Africans 2-2 Ruvu Shooting.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kuwaingiza Shamte Ally, Juma Seif na Hamis Kiiza waliochukua nafasi za Rashid Gumbo, Juma Abdul na Jeryson Tegete.
Mabadiliko hayo yaliiongezea Yanga uhai kwani katika dakika ya 65, mshambuliaji Didier Kavumbagu aliipatia bao la tatu na kufikisha jumla ya mabao manne katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Yanga iliendelea kukosa mabao ya wazi kupitia kwa washambuliaji wake Hamis Kiiza na Shamte Allly ambao hawakua makini katika umaliziaji.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africasn 3 - 2 Ruvu Shooting.
Matokeo hayo yanaipeleka Young Africans mpaka katika nafasi ya 3 ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kufikisha point 14.
Yanga itacheza na Polisi Morogoro siku ya jumatano Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara 2012/2013.
Yanga : 1.Yaw Berko, 2.Juma Abdul/Juma Seif Kijiko, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Mbuyu Twite, 6.Rashid Gumbo/Shamte Ally, 7.Nurdin Bakari, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu, 10.Jeryson Tegete/Hamis Kiiza, 11.David Luhende
<
0 comments:
Post a Comment