
Timu ya taifa ya Ujerumani imelazimishwa sare ya magoli 4-4 na timu ya taifa ya Sweden ukiwa ni mwendelezo wa michuano ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa bara la Ulaya nchini Brazil mwaka 2014.IIlikuwa ni mechi nzuri sana na ya kusisimua kwani mpaka dakika ya 55 Sweden walikuwa nyuma kwa magoli 4-0 lakini walipigana na kusawazisha na hivyo kufanya pambano kuisha kwa sare ya magoli 4-4.
Alikuwa ni Rasmus Elm aliyeisawazishia Swedwn goli la nne katika dakika ya 93 na hivyo kuitimisha rekodi ya Ujerumani ya ushindi wa 100% katika kundi C katika jiji la Berlin.Zlatan Ibrahimovich,Mikael Lustig na Johan Elmander walifunga ndani ya dakika 14 kabla ya Rasmus Elm kusawazisha na hivyo kufanya matokeo kuwa 4-4 mpaka mwisho wa mchezo.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Sweden Erik Hamren anasema kuwa "ni pambano la kihistoria ambalo lilikuwa na hisia nyingi sana na mashabiki walipata burudani kubwa"anamalizia kocha Erik wa Sweden.
Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Miroslav Klose (2),Per Mertesacker na Mesut Ozil.
0 comments:
Post a Comment