
Shirikisho la soka barani Afrika(CAF) limeifungia timu ya taifa ya Senegal kutokana na vurugu zilizotokea siku ya jumamosi katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.Katika adhabu hiyo,CAF wameifungia timu ya Senegal kutoshiriki kwa fainali za mwakani nchini Afrika Kusini alhali tayari mpaka pambano lao dhdi ya Tembo wa Ivory Coast likiwa limeshaipa timu ya Ivory Coast ushindi wa jumla wa magoli 6-2.
Na katika hatua nyingine shirikisho hilo la kabumbu barani Afrika limesema kuwa ushindi walioupata timu ya taifa ya Ivory Coast wa magoli 2-0 kabla ya pambano kuvunjika kutokana na vurugu za mashabiki utabaki pale pale wa magoli 2-0.
0 comments:
Post a Comment