Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, October 15, 2012

CAF YATOA MPANGILIO WA MAKUNDI KUELEKEA MATAIFA YA AFRIKA

Chisamba Lungu of Zambia
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa mpangilio wa makundi utakavyokuwa katika kueleka fainali za mataifa hayo ya Afrika nchini Afrika ya Kusini mwakani 2013.Katika mpangilio huo zimo timu za Ivory Coast ambayo ilicheza na Senegal katika mechi ya kufuzu kwa fainali hizo na mechi hiyo kutawaliwa na vurugu za mashabiki wa Senegal.Pia zipo timu za Cape Verde ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza kunako fainali hizo mara baada ya kumtoa kigogo Camerron katika pambano lililowashangaza watu wengi mno.

Wamo pia wenyeji Afrika ya Kusini ambao wao wanaenda moja kwa moja kama mwenyeji.Pia bila kuwasahau Ethiopia ambao nao wamefuzu baada ya kuwafunga jirani zao Sudan na hivyo kushiriki kwa mara ya pili baada ya kipindi cha miaka 30 tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwaka 1982.
Makundi ya fainali hizo yatatangazwa 24 October 2013 huku fainali hizo zikianza January 19 mwakani mpaka 10 February.
Mpangilio wa makapu hayo kwa timu shiriki upo kama ifuatavyo;


  • Kapu No 1. South Africa, Zambia, Ghana, Ivory Coast
  • Kapu No  2. Mali, Tunisia, Angola, Nigeria
  • Kapu No  3. Algeria, Burkina Faso, Morocco, Niger
  • Kapu No. 4. Togo, Cape Verde, DR Congo, Ethiopia.

0 comments:

Post a Comment