
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo atatimiza mechi 100 kesho za kimataifa akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno katika pambano la kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Ireland ya Kaskazini.Ronaldo aliyeanza maisha yake ya soka kama beki wa kati kabl ya kubadili nafasi hiyo na kuwa mshambuliaji atakuwa mchezaji wa tatu kunako kikosi hicho cha Ureno kufikia mechi 100 akiwa sambamba na wachezaji wa zamani waliofikisha idadi hiyo kama Luis Figo mechi (127) na Fernando Couto(110).

"Nina furaha sana kutimiza idadi ya mechi hizo 100 na hakika najivunia kuichezea timu ya taifa langu" anasema Cristiano Ronaldo.Ronaldo ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid anatarajiwa kuiongoza Ureno katika mechi ya kesho dhidi ya Ireland ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment