Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, October 25, 2012

NITATUMIA UZOEFU WANGU KATIKA MICHUANO YA AFRIKA-LE ROY



Baada ya ratiba kupangwa hapo jana,kocha wa timu ya taifa ya Congo Claude Le Roy amesema kuwa ana uzoefu wa kutosha katika kufundisha soka barani Afrika hivyo haziogopi timu alizopangwa nazo katika michuano hiyo.Akizungumza mara baada ya ratiba ya michuano hiyo ya Afrika kocha huyo alisema kuwa anajua timu yao ya Congo ipo katika kundi gumu lakini ana imani ya kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Congo wapo kuni B pamoja na timu za Niger,Mali na Ghana.Akiizungumzia Ghana kocha Le Roy anasema kuwa "naifahamu vizuri Ghana kwani nimeshawahi kuifundisha ndiyo maana hata Rais wa chama cha soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi alinipigia simu mara timu yangu ya Congo ilipopangwa kundi moja na Ghana akisema kuwa hakupenda kukutana nami kwani nawafahamu vizuri sana".

Claude Le Roy aliifundisha Ghana kati ya mwaka 2006-2008 na kocha msaidizi wa Ghana Maxwell Konadu alisikika akikiambia moja kati ya vituo vya Radio kuwa Le Roy anawafahamu karibu wachezaji wengi wa sasa wa Ghana walio timu ya Taifa.

0 comments:

Post a Comment