
Mashabiki wa klabu ya soka ya National Al Ahly wameruhusiwa kuangalia gainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya timu ya Esperance Du Tunis ya nchini Tunisia.Mashabiki hao ambao wanasifika kwa vurugu katika viwanja hasa vya nyumbani nchini Misri watakuwa mashuhuda wa fainali hiyo tangu kufungiwa kwao kuingia uwanjani mwezi wa pili mwaka huu(2012).Al Ahly watakuwa wenyeji wa klabu ya Esperance ya Tunisia Novemba 4 katika uwanja wa Borj El Arab kunako mji wa Alexandria ikiwa ni mara ya kwanza tangu kufungiwa kwa mashabiki hao baada ya tukio lililotokea Port Said mwezi wa pili mwaka huu.
Kuelekea pambano hilo Rais wa Misri Mohammed Mursi amezitaka familia wahanga wa tukio la Port Said kujitokeza uwanjani katika kuishangili timu ya Al Ahly na kuhaidi kuwa tukio lililotokea wakati ule halitojirudia tena.Takribani watu 30,000 wanatazamiwa kuwepo uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wa National Al Ahly katika fainali hiyo ya kwanza itakayofanyika nchini Misri.
0 comments:
Post a Comment