Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, October 30, 2012

NIPO TAYARI KUIUZA AC MILAN-BERLUSCONI

 
Mmiliki wa klabu ya AC Milan Slvio Berlusconi anasema kuwa yupo tayari kuiuza klabu hiyo ya jiji la Milan katika maeneo ya Lombard endapo atapata ofa nzuri toka kwa mfalme wa Emir kunako utawala wa Arab Emirates Sheikh Hamad Bin Halifa Al Thani.Kauli hiyo inakuja siku chache wakati ambapo Mahakama Kuu ya nchini Italia ikimhukumu Berlusconi kwenda jela kwa mwaka mmoja kutokana na kashfa ya ukwepaji kodi nchini humo.

Klabu hiyo kwa sasa inakabiliwa na matatizo makubwa sana ya kiuchumi na hivyo kupelekea kuuzwa kwa nyota wake kama Thiago Silva na Zlatan Ibrahimovic waliotimkia (PSG) wakati nyota wengine kama Clarence Seedorf,Gennaro Gattuso na Alessandro Nesta wakioneshwa milango ya kutokea ili kupunguza mishahara mikubwa ya wachezaji hao waliokuwa wakiipata klabuni hapo.Berlusconi anaweza kuiuza Milan kwa kiasi cha euro 500milioni kama waarabu hao watakubali kumpa kiasi hicho cha fedha.Pia makampuni kama Gazprom na Ferrero yameonesha nia ya kuinunua klabu hiyo ya Milan.


0 comments:

Post a Comment