Uganda,Kenya,Tanzania,Burundi,Rwanda,Eritrea,Sudan Kusini na Sudan Kaskazini na nchi nyingine waalikwa kama Zambia kama watathibitisha kushiriki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Akizungumzia mipango ya timu hiyo ya taifa ya Somalia,katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu la nchini humo Somali ndugu Abdi Qani Said Arab anasema kuwa "uwanja wa taifa kwa sasa upo chini ya ukarabati kwa msaada wa FIFA na uwanja mwingine uliopo Mogadishu unatumiwa na majeshi ya umoja wa Afrika katika kulinda amani hivyo itatulazimu kuwahi kufika Uganda mapema na kuwa na muda mrefu kidogo wa maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano yenyewe",anasema Abdi.
Timu hiyo inatarajia kuwasili nchini Uganda mnamo Novemba 8 na kuweka kambi ya muda wa siku 15 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza tarehe 24 Novemba mwaka 2012.Katika kuonesha dhamira ya kufanya vizuri safari hii,Somalia imewaita wachezaji saba toka nchi za nje huku wachezaji wawili wakitoka Uingereza,wawili wakitoka Marekani,wawili wakitoka Uholanzi na mmoja akitoka nchi ya Kuwait.
0 comments:
Post a Comment