Hii hapa ni rekodi ya mwamuzi huyo tangu apandishwe daraja mwaka 2004 akiingia katika mchujo wa marefa watakaochezesha Ligi Kuu England na baadaye kuingia rasmi kama refa mwaka 2005 katika Ligi hiyo yenye utajiri mkubwa sana ulimwenguni.
- Mwaka 2005 alishindwa kutoa maamuzi sahihi juu ya goli alilofunga Pedro Mendes ambapo mpira ulivuka mstari wa goli huku kipa wa Manchester United Roy Carroll akiutolea wavuni katika pambano kati ya Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspurs mechi ikifanyika Old Traffford.Tukio hilo halikumfanya Mark kutochaguliwa katika orodha ya marefa bora wa FIFA mwaka 2006.
- Mwaka 2008 mnamo mwezi wa nane,mwamuzi huyo Mark Clattenburg alifungiwa na Bodi ya Chama Cha Maofisa wa Ligi Kuu ya soka nchini England(Proffesional Game Match Officials Board) kutokana na uchunguzi uliofanyika na kumkuta mwamuzi Mark akiwa na tuhuma za kumiliki fedha isivyo halali kiasi cha fedha za Ulaya (euro 60,000).
- Mwezi Februari mwaka 2009 mwamuzi Mark alikata rufaa ya adhabu aliyopewa kutokana kufungiwa na Bodi ya kamati ya Ligi nchini England ya kufungiwa kwa muda usiojulikana lakini shauri lake lilikataliwa na hivyo kufungiwa miezi nane ya kutochezesha Ligi za England.
- Mwaka 2009 meneja wa Manchester City Mark Hughes alimtolea maneno makali mwamuzi huyo kwa kitendo chake cha kumtoa nje mshambuliaji Craig Bellamy katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Bolton.Ukiwa mwaka haujaisha mwamuzi huyo alimsikitisha kocha wa zamani wa Tottenham mara baada ya kukubali goli la winga wa Manchster United Luis Nani dhidi ya timu ya Tottenham goli lililokuwa na utata mkubwa sana.
- Katika mechi hiyo kipa wa Tottenham Heurelho Gomez aliweka mpira chini kwa lengo la kuupiga mbele mara baada ya kuudaka kilichotokea ni kwamba winga wa Man United Nani aliiufata na kuupiga golini na mwamuzi Mark aliuelekeza mpira katikati ya uwanja kuashiria kuwa ni goli.
- Cha kushangaza ni kuwa mwamuzi huyo kila anapofanya kosa kubwa huwa na bahati ya kupewa mechi nyingine kubwa zaidi.Kwa mfano; mwamuzi Mark Clattenburg alichezesha mechi ya Fainali kati ya Liverpool na Cardiff City mwezi wa pili mwaka huu(2012) na pia bila kusahau mechi ya Fainali ya Olympic ya wanaume kati ya Brazil dhidi ya Mexico iliyofanyika mwezi wa nane mwaka huu(2012).
Rekodi nyingine za mwamuzi wa Mark Clattenburg.
- 2012-13 - Mechi: 9; Yellows: 40; Reds 4
- 2011-12 - Mechi: 36; Yelows: 115; Reds: 8
- 2010-11 - Mechi 40; Yellows: 123; Reds 7
- 2009-10 - Mechi: 42; Yellows: 105; Reds: 5
0 comments:
Post a Comment