Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, October 10, 2012

NI ARGENTINA DHIDI YA URUGUAY

Kama kuna mechi ya wapinzani wa jadi ambayo huwa inavuta hisia za watu wengi katika soka basi ni mechi inayohusisha timu za taifa ambazo ni Argentina dhidi ya Uruguay.Upinzani huu haukuanza hivi karibuni bali ni karne kwa karne na hakika miamba hii miwili inapokutana basi nyasi huumia sana.

Katika kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil,bara la Amerika ya Kusini nalo litaendelea na ratiba yake ya michuano ya kufuzu kwa kombe hilo la dunia na takribani mechi kadha wa kadha zitapigwa likiwemo pambano la kukata na shoka kati ya Argentina dhidi ya Uruguay.

Timu hizi zimeshakutana mara 178 huku Argentina akiibuka na ushindi mara 83,akitoka sare mara 41 na kupoteza mechi 54.Argentina imefunga jumla ya magoli 287 dhidi ya 214 ya Uruguay kwa mara zote walizokutana.

Zifuatazo ni mechi bora za wapinzani hawa wa jadi zinazojulikana kama 'River Plate' derby.

Uruguay 0-6 Argentina
 Mwaka 1902 / 20July
Montevideo- mechi ya kirafiki
Mechi ilichezwa katika mji mkuu wa Uruguay Montevideo ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha magoli 6 kwa 0 dhidi ya mahasimu wao  Argentina.Ulikuwa ni ushindi mkubwa kuwahi kutokea wakati timu hizo zilipokutana.Ndizo timu zilizokutana mara nyingi zaidi katika historia ya mpira wa miguu duniani.

Uruguay 4-2 Argentina
Fainali ya mwaka 1930 katika nchi ya Uruguay huku timu hiyo ikiibuka na ushindi wa magoli 4-2.Pambano hilo likifanyika katika uwanja uliojulikana kama 'Estadio Centenario,Montevideo'.
Magoli ya Carlos Paucelle na Guillermo Stabile yaliifanya Argentina iongoze kwa magoli 2-1 mpaka mapumziko.Lakini kipindi cha pili kilishuhudia Uruguay wakijibu mapigo na kusawazisha kupitia kwa wachezaji wake Pablo Dorado,Pedro Cea,Victoriano Iriarte na Hector Castro na kuifanya Uruguay iibuke kidedea katika fainali hiyo na kuwa mabingwa wa kwanza  wa kombe la dunia.

Argentina 1-0 Uruguay
Ilikuwa ni raundi ya 16 ya Fainali ya kombe la iliyofanyika Mexico 1986 katika uwanja uliojulikana kama 'Estadio Cuauhtemoc,Puebla.
Wakimtupia macho zaidi mshambuliaji nyota Diego Maradona na kuwasahau wachezaji wengine kama Pedro Pablo Pasculli aliyekuwa akiichezea Lecce  ambaye ndiye aliyekuwa shujaa wa mechi hiyo kwa kuipa Argentina goli pekee la ushindi.

Uruguay 0-1 Argentina
14 mwezi wa kumi 2009.Kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini katika kanda ya Amerika ya Kusini.Pambano likifanyika 'Estadio Centenario,Montevideo'.
Mario Bollati ndiye alikuwa shujaa wa Argentina akifunga goli pekee la ushindi kwa timu hiyo ikiwa ni miaka 33 tangu Argentina waifunge Uruguay nchini mwake katika jiji la Montevideo.Akitokea benchi kama mchezaji wa akiba na kufanikiwa kufunga katika dakika ya 79.Argentina ilikuwa chini ya kocha Diego Maradona wakati wa kufuzu kwa fainali hizo za kombe la dunia.

Argentina 1-1 Uruguay(Uruguay yashinda kwa penati 5-4).
Robo fainali ya Copa America tarehe 16 July 2011 pambano likipigwa katika uwanja wa Brigedier Estanislao Lopez,Santa Fe.
Baada ya magoli ya Diego Perez kwa upande wa Uruguay na ambaye  baadaye alitolewa kwa kadi nyekundu na huku Gonzalo Higuain akiisawazishia Argentina mchezo huo uliendelea mpaka katika hatua ya matuta.

Bila kusahau zipo mechi nyingine nzuri zilizowakutanisha wababe hawa wa Amerika ya Kusini katika mwaka 1928 katika FIFA/Olympic na ile ya mwaka 1987 katika ile nusu fainali ya Copa America ambayo inatajwa kama mechi iliyokuwa bora na ya kusisimua ambapo Uruguay ilishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Argentina katika nusu fainali iliyofanyika Buenos Aires.

0 comments:

Post a Comment