Kiungo mshambuliaji Marouane Fellaini atakuwa nje kwa wiki 3 mpaka nne kutokana na kuumia kifundo cha mguu.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye alipatwa na matatizo hayo katika mechi ya klabu yake ya Everton dhidi ya Wigan jumamosi iliyopita atakosa mechi za kimataifa za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Serbia na Scotland wiki hii.
0 comments:
Post a Comment