
Serikali ya Zambia imewahaidi wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo kiasi cha dola za kimarekani USD $ 5,000 kwa kila mchezaji endapo timu hiyo itaifunga timu ya taifa Uganda ama 'The Cranes' katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika katika pambano litakalofanyika nchini Uganda kunako uwanja wa Namboole kunako mji wa Kampala.
Akizungumzia kuhusu suala hilo waziri wa michezo wa Zambia Chishimba Kambwili amesema kuwa kila mchezaji atapata kwacha K25.5 ambayo ni sawa na dola 5,000 za kimarekani.Kawaida kila mchezaji hupata K15.5 ambazo ni sawa na dola 3,000 za kimarekani lakini Serikali ya Zambia kwa kuona umuhimu wa mechi hiyo,Serikali hiyo imeona jambo la maana kuwaongezea dola 3,000 kama sehemu ya motisha katika mechi hiyo ya kufuzu katika mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika ya Kusini.
0 comments:
Post a Comment