
Klabu ya Manchester United jana iliendeleza wimbi la ushindi mara baada ya kuifunga timu ya Stoke City kwa magoli 4-2.Stoke ndiyo walikuwa wa kwanza kuzina nyavu za Man United mara baada ya mchezaji Wayne Rooney kujifunga katika dakika ya 11 kabla ya kusawazisha makosa katika dakika ya 27 kwa kuisawazishia Man United kwa goli la kichwa akiunganisha krosi ya Robin Van Persie.

Dakika ya 44 Robin Van Persie aliwainua mashabiki wa Man United katika viti vyao kwa kufunga goli la pili akiunganisha krosi ya Antonio Valencia.Danny Welbeck aliongeza goli la 3 katika dakika ya 46 mara baada ya mapumziko akiunganisha krosi ya Rooney kabla ya Rooney kusherehekea vyema miaka yake 10 ya Ligi Kuu ya soka nchini England kwa kufunga goli lake la pili la mchezo huo katika dakika ya 65.Rooney alianza kucheza Ligi hiyo mwaka 2002 Oktoba ya 19 katika pambano kati ya Everton na Arsenal wakati huo akiichezea Everton.

Stoke walipata goli lao la pili la mchezo kupitia kwa Kightly dakika ya 58 na mpaka mwisho wa mchezo Mna United waliibuka na ushindi wa magoli 4-2.
0 comments:
Post a Comment