
Alikuwa ni kiungo mshambuliaji kunako kikosi hicho Chelsea 'The Blues' Juan Mata ambaye aliiwezesha klabu ya Chelsea kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka nchini England mara baada ya kuiwezesha klabu hiyo ya darajani kuibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya timu ya Tottenham Spurs.

Chelsea walikuwa wa kwanza kufunga kwa goli la beki wake Gary Cahill kabla ya William Gallas kusawazisha.Jermain Defoe aliongeza tena goli la pili kwa upande wa Spurs lakini Juan Mata alisawazisha kabla ya kuongeza goli lingine na kinda Daniel Sturidge kukamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli la nne na hadi filimbi ya mwisho matokeo yalikuwani Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 4-2.

0 comments:
Post a Comment