Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, October 30, 2012

MAN CITY YAZIDI KUIMARISHA BENCHI LAKE LA UFUNDI

Klabu ya Manchester City imezidi kuimarisha benchi lake la ufundi mara baada ya kumchukua aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya FC Barcelona Txiki Begiristain kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Brian Marwood kwa muda mrefu sana.Txiki anakuwa ni afisa wa pili wa ngazi za juu toka klabu ya Barcelona kujiunga na Manchester City mara baada ya aliyekuwa kiongozi wa Barca Frank Sorano kujiunga kama Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Manchester City mwaka huu.

Txiki alizaliwa mwaka 1964 tarehe ya 12 Agosti.Katika maisha yake ya kucheza kabumbu, Txiki alivichezea vilabu vya Real Sociedad(1982-1988) mechi 187 huku akifunga magoli 23,pia aliichezea klabu ya Barcelona mwaka(1988-1995) mechi 223 huku akifunga magoli 63 akiwa kama winga na muda mwingine akicheza kama mshambuliaji wa kati.Pia alivichezea vilabu vya Deportivo La Coluna kabla ya kumalizia soka lake nchini Japan kwa kuchezea timu ya Urawa Reds ambapo alistaafu soka mwaka 1999.Txiki alijunga na Barcelona kama Mkurugenzi wa ufundi mwaka 2003 ambapo alidumu katika nafasi hiyo kwa miaka saba mpaka mwaka 2010.

0 comments:

Post a Comment