Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, October 10, 2012

BA,CISSE NA BEN HARFA KUTOVAA UZI WA MDHAMINI MPYA


Wakiongozwa na 'Sharia' ya kiislamu,wachezaji Demba Ba,Pappis Demba Cisse,Haterm Ben Harfa na Cheikh Tiote wamesema kuwa itawawia vigumu sana kwa wao kuvaa jezi za mdhamini mpya kampuni inayojulikana kama Wonga.com.Kampuni hiyo iliyosaini mkataba na  klabu hiyo ya Newcastle United kwa muda wa miaka minne imekuwa ikifanya kazi za ukopeshaji fedha kwa taasisi mbalimbali na hivyo kujiendesha kifaida zaidi kutokana na marejesho ya fedha kwa Riba inayotokana na mikopo wanayotoa kwa taasisi au makampuni mbalimbali.

Kutokana na shughuli za kampuni hiyo,wachezaji hao wenye imani  ya dini ya kiislamu wameona itakuwa busara kama wao hawatokuwa sehemu ya uvaaji wa jezi za klabu hiyo msimu ujao ambazo zitakuwa na nembo ya mdhamini huyo.Sharia ya Kiislamu inasema kuwa"Muisalmu au Waisalmu wasifaidike na faida yoyote inayotokana na wao kutoa au kupokea fedha toka sehemu yoyote ile".Kwa maana nyingine Riba hairuhusiwi katika dini ya Kiislamu.

Sakata la wachezaji hao linafanana na lile la mchezaji wa zamani klabu za Tottenham na West Ham United Fredrick Kanoute ambaye naye aligoma kuvaa jezi za mdhamini wa klabu ya Sevilla kampuni ya Bet 888 ya nchini Hispania kutokana na mdhamini huyo kujihusisha na kamari katika kujiendesha kama kampuni.Badala yake Kaoute alivaa jezi isiyokuwa na mdhamini na katika mechi za Ligi na mechi nyinginezo ingawa alikubali kuvaa jezi za mdhamini huyo wakati wa mazoezi.

Sheikh wa baraza kuu la Waislamu katika nchi ya Uingereza hakuwa mbali kulizungumzia hilo kwa kusema kuwa"Kuna mambo mawili katika hilo ambayo ni kufuata Sharia ya Kiislamu kama inavyosema au kufuata kile ambacho mtu  anachoona ni sahihi kwake".Lengo la yote ni kuwalinda watu na unyonyaji huu wa matajiri ulimwenguni.Sakata hili limeendelea kuchukua sura tofauti katika mji wa Newcastle kwa maana ya kutaka kujua kama wachezaji hao wenye imani ya dini ya Kiislamu watabakia na msimamo huo wa kutovaa jezi za mdhamini au watavaa lakini kwa masharti ya kuvaa jezi wakati wa mazoezi tu na siyo kwenye mechi.

0 comments:

Post a Comment