
Akiiongoza England katika pambano dhidi ya San Marino nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney alifunga mara 2 katika ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya timu ya San Marino katika michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

England waliweza kupata magoli yake kupitia kwa nahodha Wayne Rooney katika dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati,na dakika ya 70 baadaye,magoli mengine yalifungwa na Danny Welbeck katika dk ya 37 na 72 na kinda mwingine Alex Oxlayde Chamberlaine dakika ya 77.
0 comments:
Post a Comment