Goli la mwisho alilofunga beki wa pembeni Jordi Alba lilitosha kuipa klabu ya Barca ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya Celtic ya nchini Uskochi.Celtic walianza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji Giorgios Samaras kabla ya baadaye kutolewa kutokana na kuumia vibaya sana.Barca walisawazisha goli lao kupitia kwa kiungo Andres Iniesta kabla ya Jordi Alba kufunga goli la ushindi.
0 comments:
Post a Comment